Sunday, May 3, 2009

Kunradhi wadau wa Simba S.c

Kutokana na maoni na ushauri toka kwa wadau wengi, kuanzia leo tarehe 4 May 2009, Blog yetu wapenzi na mashabiki wa Simba itabadilishwa jina na kuwa:
www.simbasportsclubfans.blogspot.com
na email itakuwa simbafans@ymail.com
Tunaomba radhi kwa usumbufu utakaotokea, hasa kwa mdau Malima aliyejiandikisha kama Follower na wadau wengine ambao maoni yao yatapotea. Hii ni kwa ajili ya maboresho!

Blog hii ya awali itaendelea kukaa kwa mwezi mzima ili kuwafahamisha watu wote kuhusu mabadiliko lakini haitakuwa na habari mpya.

Kikosi Cha Simba 2008 / 09

Kipa: Ally Mustapha*, Deo Mushi*, Amani Simba
Beki: Salum Kanoni, Juma Jabu, Ramadhan Chollo, Ramadhan wasso, Juma Nyoso, Kelvin Yondani*,Meshack Abel*, Deo Naftari, Victor Costa.
Viungo: Henry Joseph*, Nico Nyagawa (capt.), Jabir Aziz*, Haruna Moshi*, Ulimboka Mwakingwe, Ramadhan Chombo
Washambuliaji: Mussa Mgosi*, Moh’d Kijuso, Emeh Izechukwu (Nigerian), Orji Orbinna (Nigerian), Moses godwin

* - walioitwa karibuni katika timu ya Taifa

Dewji akata mzizi wa fitna

Hatimae mwenyekiti wa kamati ya Usajili ya Simba, Kassim Dewji ameweka wazi kuwa hawatakuwa tayari kumsajili tena kipa JUma Kaseja, bali watawaendeleza waliopo sasa kwa kuwa wana uwezo mkubwa." Tumeamua kumwachia mwalimu Phiri achague wachezaji wote anaotaka kuwasajili na sisi tunachofanya ni kumpa mapendekezo tu. Lakini atakapoleta suala la Kaseja tutamwambia NO".
Pengine maoni ya wadau wa globu hii yamechangia kufikisha ujumbe kwa viongozi, tukaze kamba kuendelea kushauriana kwa manufaa ya timu yetu

Special kwa Mdau wa Ughaibuni

Kikosi cha Simba kilichoshika nafasi ya pili katika msimu huu 2008/09/ Mwenye suti ndiye Coach mkuu Patrick Phiri.Bahati mbaya timu zetu hazina utamaduni wa kupiga picha ya pamoja na wachezaji wote waliosajiliwa ktk msimu n kuziuza.Hii ingeweza hata kuongeza kipato kidogo.

Saturday, May 2, 2009

Basi za TBL


Mwenyekiti wa Simba akipokea mabasi toka kwa Mkurugenzi wa masoko wa TBL, D.Minja.

Friday, May 1, 2009

TBL waikabidhi Simba Sc. Mabasi 2

Mdhamini mkuu wa timu ya Simba, TBL kupitia bia yake ya Kilimanjaro leo wamewakabidhi Simba Mabasi 2 (Toyota Coaster 'mayai' na Toyota Hiace) kwa ajili ya matumizi ya shughuli za club!Kwa ujumla mabasi hayo yana thamani ya karibia Milioni 100 (kwa mujibu wa wadhamini).
Picha za mabasi hayo zitatoka soon! Watani wetu nao wamepewa mabasi kama sisi
Asante TBL

Fununu za Usajili

Kuna fununu kuwa Simba imemnasa kiungo wa kulia wa Yanga, Shamte Ally katika usajili wake. Habari hii bado ni fununu na haijathibitishwa na uongozi wala mchezaji mwenyewe.

Kaduguda amwaga cheche

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Katibu Mkuu wa klabu hiyo Mwina Kaduguda (pichani), alisema kuwa uongozi wao umejipanga kuhakikisha timu inarudisha makali yake kama ya mwaka 2003 na kufikia hatua za juu za michuano ya kombe la Shirikisho. Kaduguda, alisema kuwa Simba ndio timu pekee yenye uwezo wa kufanya vizuri kwenye michuano ya kimataifa hapa nchini, ambapo rekodi yake haijawahi kuvunjwa.


"Tumeshindwa kuiwakilisha nchi kwa zaiaid ya mwaka mmoja, kipindi tulichokuwa nje kimetufundisha mengi, nina imani tutarudi na nguvu mpya,"alisema Kaduguda

Comment: Tunawatakia viongozi wetu kila la Kheri

Simba Vs Zanzibar Heroes Kesho

Timu ya Simba kesho itajipima na timu ya taifa ya Zanzibar, Zanzibar Heroes katika mchezo ulioandaliwa na TASWA. Ikumbukwe kuwa awali Simba ilipangwa kucheza na wachezaji wa nje ya TZ wanaocheza ligi kuu lakini wachezaji hao wanaoongozwa na wachezaji wengi wa Yanga wameingia mitini. Simba itakipiga bila wachezaji wao wote nyote walioko kambini na timu ya Taifa.
Kila la Kheri

Phiri kusaka vipaji mikoani

Kocha mkuu wa Simba, Mzambia Phiri amesema atazunguka nchi nzima kusaka wachezaji wa kukiongezea makali kikosi cha Simba.

“Nitazunguka mikoa mingi ya Tanzania ili kupata wachezaji watakaoweza kuisaidia timu yangu kucheza msimu ujao kwa ufanisi, si kwamba sina wachezaji mahiri...ukweli ni kwamba nataka kuwa na timu bora zaidi,” Alisema Phiri.

Comments: Hivi hatujafikia wakati wa kutumia Scouts kusaka wachezaji mikoani wakamletea kocha akawafanyia majaribio?Hata tukiamua kumlipa commission kidogo yule ambae mchezaji wake atasajiliwa, nadhani itasaidia sana. Halafu klabu yetu iimarishe timu ya vijana, sio kuokoteza wachezaji.tuyatumie mashindano ya Copa Cocacola kusajili timu imara ya vijana ambao tutawasajili na hata kuwauza nje kwa kuwa umri wao unaruhusu.

Thursday, April 30, 2009

Harakati za usajili zaanza!

Simba imeanza harakati za usajili wa wachezaji kwa ajili ya msimu ujao huku panga likielekea kuwapitia baadhi ya wachezaji wakiwamo Wanigeria Emeh Izichukwu na Orji Obinna.
Habari za uhakika kutoka ndani ya klabu zinasema, wengine walioko katika hatari ya kupitiwa na mchujo huo ni beki mzoefu Ramazan Wasso na kipa Amani Simba.

Simba imeamua kuwa msimu ujao inataka kusajili wachezaji wachache ambao watalipwa vizuri na kuachana na tabia ya kuwa na wachezaji wengi ambao hawatumiki na badala yake wamekuwa wakikaa benchi kwa msimu mzima.

Habari toka klabuni zinasema, wachezaji wengi wa msimu uliopita hasa wale nyota wamekuwa wakivurunda katika mechi nyingi na nia yao ni kuwapunguza na kumwachia kocha Patrick Phiri kusajili kikosi ambacho kitaleta mabadiliko.

Comments; Mi nadhani ule wakati wa viongozi / wafahili kusajili kila mtu mchezaji wake umepitwa na wakati. Kocha aamue anataka wachezaji gani, timu itafute pesa wasajiliwe.Sio ooh, huyu mchezaji wa kundi hili, huyu kaletwa na fulani...hapo hatujengi, tunabomoa timu. Halafu foreign player akisajiliwe awe na vitu tofauti na wa ndani, sio mtu kama Wasso!

Tuesday, April 28, 2009

Jamaa walipoponea tundu la sindano

Redondo akishangilia goli la kwanza alilowafunga Yanga katika mechi ya marudiano. Bahati yao refa aliwabeba kwa kuwaongezea dakika 7.

Monday, April 27, 2009

Juma Kaseja arudishwe Simba

Kama habari kuwa viongozi wa Simba wakiongozwa na Friends of Simba wana mpango wa kumrudisha tena Juma Kaseja Msimbazi. Je?Kuna umuhimu wa kutumia pesa nyingi kumsajili Juma? maana kwa sasa Ally Mustapha na Deo Dida ni makipa wazuri na wana uwezo wa kuendelea kuwa bora zaidi. Mi nadhani tungetumia pesa kusajili forward mmoja mzuri na attacking mid fielder badala ya kipa, wengine mnaonaje?

Phiri atupeleka CAF

Kama alivyoahidi alipofika, Coach Patrick Phiri ametimiza lengo lake kwa kutupeleka mashindano ya CAF kwa kupata nafasi ya pili. Ikumbukwe kuwa alikuja tukiwa tumepoteza points nyingi sana mzunguko wa kwanza. Pata habari kamili

Simba Yairarua Polisi Dodoma 2 - 0

Kwa matokeo hayo Simba sasa imekata tiketi ya kushiriki michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika (CAF), mwakani baada ya kufikisha pointi 40, huku Yanga ambayo jana pambano lao lilishindikana kufanyika kutokana na Uwanja wa Uhuru kujaa maji ikiwa mabingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom.Hadi kipindi cha kwanza kinamalizika, hakuna timu iliyoweza kuona lango la mwenzake licha ya mpira kuwa wa kasi kubwa, huku timu zote zikishambuliana kwa zamu.Kipindi cha pili kilianza kwa kasi, huku Simba ikishangiliwa na umati wa mashabiki waliokuwa wamefurika uwanjani hapo, katika dakika ya 70, alikuwa ni Haruna Moshi 'Boban' aliyeanza kuwanyanyua mashabiki wa Wekundu wa Msimbazi kwenye viti baada ya kupachika bao safi.Baada ya dakika 12 baadaye, alikuwa ni Mohammed Kijuso aliyeihakikisha Simba kushiriki michuano ya CAF mwakani baada ya kuiandikia bao la pili na la ushindi, huku Polisi Dodoma ikikata tiketi ya kushuka daraja.Mara baada ya mchezo huo kumalizika, Katibu Mkuu wa Chama cha Mkoa wa Singida (SIREFA), Hussein Mwamba, aliliambia gazeti hili kuwa, Simba itaondoka Dodoma (Jumatatu) leo, kuelekea Singida kwa ajili ya kucheza mechi moja ya kirafiki dhidi ya Timu ya Mkoa huo, Singida Shooting Stars

Karibuni

Karibuni mashabiki na wapenzi wote wa timu ya Simba Sports Club 'Mnyama' tupashane habari, kubadilishana mawazo na hata kukosoana katika blog yetu.